KUKAMATWA KWA MFANYAKAZI NCHINI MAREKANI BAADA YA KUVUJISHA SIRI
Idara ya Sheria ya Marekani imetangaza Jumatatu kukamatwa
kwa mfanyakazi aliyeajiriwa kwa mkataba serikalini ambaye inasemakana alituma
taarifa za siri kwenye kituo cha habari kinachotumia mtandao.
Tangazo hilo limetokea siku hiyo hiyo wakati repoti ya
kukamatwa kwa uvujishaji wa siri hiyo, ikisema kuwa nyaraka za siri
zilizokamatwa zinaonyesha kuwa idara ya usalama katika jeshi la Russia
ilijaribu kuingia katika mfumo wa usajili wa kura wa Marekani kabla ya uchaguzi
wa mwaka jana.
Waraka wa kiapo uliokabidhiwa na afisa maalum wa FBI umesema
kuwa mwanamke aliyekamatwa, Reality Leigh Winner, amekiri kuwa alidukua repoti
hiyo ya usalama ya siri na kuituma kwa taasisi ya habari.
Kiapo hicho pia kinaeleza kwamba shirika la jumuiya ya
usalama ya Marekani wametambua katika uchunguzi wao kuwa watu sita walichapisha
nyaraka hiyo, akiwemo Winner, na kuwa alikuwa na mawasiliano ya email na
taasisi ya habari iliyokuwa haijatajwa jina.
Tarehe zilizokuwa katika nyaraka zote zilizotajwa kwenye
kiapo na ile ilionukuliwa kutokana na kukamatwa kwa udukuzi huo zinalingana.
Serikali haikusema kutoka shirika gani Winner anadaiwa
alichukua waraka huo wa siri ya juu, akisema kuwa alikuwa amepewa jukumu kufanya
kazi katika ofisi ya serikali ya Marekani katika jimbo la Georgia.

No comments: