ARSENAL KUMSAJILI BEKI WA KUSHOTO KUTOKA BOSNIA.
Arsenal wametangaza kumchukua beki wa kushoto Sead
Kolasinac mwenye umri wa miaka 23 kutoka nchini Bosnia.


Kolasinac amekuwa akiichezea klabu ya Schalke ya Ujerumani amejiunga na timu hiyo bila kulipwa pesa na atakuwa mchezaji rasmi pale soko la kuhama wachezaji litakapofunguliwa rasmi ifikapo julai 1 mwaka huu.
Schalke
wamethibitisha kwamba beki huyo ametia saini mkataba wa Arsenal ambao unadumu hadi 2022 aliisaidia
timu hiyo kumaliza nafasi ya 10 Bundesliga msimu uliopita na walifanikiwa
kufika robo fainali ya ligi la Europa ambapo waliondolewa na Ajex iliyofika
fainali.
"Arsenal ina utamaduni wa muda mrefu na niliifuatilia
klabu hii tangu nilipokuwa mvulana mdogo, enzi za Jens Lehmann na Thierry
Henry," mchezaji huyo aliambia tovuti ya Gunners.
No comments: