HATIMAYE RAIS WA NIGERIA MUHAMMAD BUHARI APATA AHUWENI.
Rais wa Nigeria Muhammad Buhari mwenye umri wa miaka 74
anaendelea vizuri akiwa hospitali ya jijini London ambako anapatiwa matibabu ya maradhi
anayougua ambayo bado hayajawekwa
bayana.

Bw. Buhari alipelekwa
hospitalini jijini humo mwezi uliopita
kwa ziara yake ya pili ya matibabu nchini Uingereza mwaka huu.
Kukosekana kwake uongozini kumesababisha mihemko nchini
Nigeria, taifa lenye uchumi mkubwa na idadi kubwa ya watu barani Afrika, huku
baadhi ya watu wakiteta kuhusiana na iwapo ataweza kurejelea kazi yake tena.
Naibu wa Rais Yemi Osinbajo anatumika kama kaimu, na
amesifiwa pakubwa kwa namna anavyoshughulikia mzozo wa kiuchumi hasa baada ya kushuka kwa bei ya mafuta bidhaa
muhimu inayouzwa kwa wingi nje ya nchi.
Mwezi Januari mwaka huu Bwana Buhari alichukua wiki saba ya
likizo ya matibabu kwenda Uingereza aliporejea nyumbani mwezi machi alisema kuwa ameongezewa damu
lakini hakufichua ugonjwa gani anaugua.
No comments: