HAZARD KUKOSA MECHI ZA MWANZO ZA MSIMU UJAO WA LIGI YA PREMIA.
Kiungo
mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard mwenye umri wa miaka 26 atakosa kucheza mechi
za mwanzo wa msimu ujao wa ligi ya Premia zitakazo anza mnamo 12 Agosti baada ya kufanyiwa upasuaji wa mfupa wa kifungo cha mguu wa kulia.
Hazard aliumia mguu
huo wakati akifanya mazoezi akiwa na
timu ya taifa ya Ubelgiji siku ya jumapili.
Hazard pia atakosa mechi
za kabla ya msimu dhidi ya Arsenal,Bayern Munich na Inter Milan zinazotarajia
kufanyika nchini Singapore kati ya tarehe 22-29 julai na mechi ya ngao ya jamii
dhidi ya Arsenal mnamo tarehe 6 Agosti.
Chelsea wamesema
kuwa upasuaji huo uliofanyika siku ya
jumatatu ulienda vyema na anatarajia kukaa kwa miezi mitatu kabla ya kuanza
kufanya mazoezi.
Hazard aliwasaidia
sana Chelsea kushinda Ligi ya Premia msimu uliomalizika majuzi ambapo
aliwafungia mabao 16 katika mechi 36.

Casinos Near Casinos Near Casinos Near Me
ReplyDeleteWe have a list of the 의왕 출장안마 10+ closest 광주광역 출장안마 casinos in Minnesota, with information about 청주 출장마사지 available 서산 출장샵 casinos near you. Find 의정부 출장샵 the closest casino to you.