ISLAMIC STATE WAMELIPUA MSIKITI NCHINI IRAQ.
Jeshi la polisi nchini Iraq limethibitisha kwamba wanamgambo
wa dola ya kiislam Islamic State (IS) wameulipua msikiti mkuu wa Al-Nuri ulioko
mjini Mosul .
Msikiti huo unaaminika ya kwamba ndimo kiongozi wa wanamgambo wa IS Abu Bakr
al-Baghdadi alitoa hotuba yake miaka mitatu iliyopita wakati alipokuwa
akitangaza "ukhalifa" mpya.
Wakati hayo yakijiri, wanamgambo hao wanadai ya kwamba ndege za jeshi la Marekani ndiyo zilizousambaratisha
msikiti huo.
Mapema leo, Kamanda wa majeshi ya Iraq amesema kuwa walikuwa mita kadhaa kutoka msikitini hapo,
walipokuwa katika harakati zao za kusonga mbele kwenye mapambano lengo likiwa
ni kuteka ngome kuu ya wanamgambo hao wa kiislam wa Is nchini Iraq.

No comments: