JAJI WA INDIA APEWA KIFUNGO
Jaji kutoka nchini India Cs Karnal ambaye amekuwa
mafichoni tangu ahukumiwe kifungo jela amekamatwa na kufungwa.
Karnan alikuwa jaji
wa kwanza wa mahakama kuu nchini India kukabiliwa na kifungo na alikamatwa katika jimbo la kusini mwa
India Tamil Nadu siku ya jumanne usiku.
Alihukumiwa kifungo mjini Kolkata huku ombi lake la
kumwachilia kwa dhamana siku ya Jumatano likikataliwa na mahakamu ya juu zaidi
.
Jaji huyo wa zamani alipatikana na hatia ya kutoa madai
dhidi ya majaji wenzake.
Alihukumiwa kwa kukaidi agizi la mahakama ya juu zaidi baada
ya kutuma barua kwa waziri mkuu Narendra Modi ambapo alimtaka kuwachukulia
hatua majaji wenzake.
Alipokonywa nguvu zake kama jaji mnamo mwezi Februari.

No comments: