CHINA KUFANYA SHEREHE YA KULA NYAMA YA MBWA
Sherehe ya kula nyama ya mbwa iliogubikwa na utata katika
mji wa Yullin nchini China ambayo hufanyika kia mwaka mkoa wa Guangxi imeanza licha ya ripoti za awali zilisema kwamba ilikuwa imepigwa marufuku mwaka huu.
Mapema mwaka huu ,wanaharakati walidai kwamba
wafanyibiashara waliagizwa na mamlaka kutouza nyama ya mbwa lakini wamiliki wa
viwanda vinavyouza nyama hiyo walisema kuwa hawajasikia lolote kuhusu hatua
hiyo kutoka kwa maafisa hao.
Mnamo tarehe 15 mwezi Mei, maafisa wa mji walithibitisha
kwamba hakuna marufuku yoyote huku Siku ya Jumatano, ripoti kutoka Yullin
zilisema kuwa mbwa waliokufa walionekana wakiwa wametundikwa katika ndoano za
nyama katika vibanda ndani ya soko la Dongkou ambalo ndio kubwa mjini humo.
Mwanaharakati mmoja alise kwamba alikatazwa na maafisa wa
polisi kuingia katika soko la Dashichang ambapo inaaminika mbwa walikuwa
wanauzwa.
Katika sherehe za miaka ya nyuma kumekuwa na mzozo kati ya
wauzaji nyama ya mbwa na wanaharakati waliojaribu kuwaokoa mbwa waliopangiwa
kuchinjwa.

No comments: