TANZANIA YAILAUMU KENYA KWA KUPIGA MARUFUKU UUZAJI WA GESI YA KUPIKIA
Serikali ya Tanzania imelalamika kuhusu hatua ya Kenya
kukataa kuruhusu wafanyibiashara wa Tanzania kuuza gesi ya kupikia nchini humo.
Kulingana na taarifa iliotolewa na katibu wa kudumu katika
wizara ya biashara na uwekezaji Profesa Adolf Mkenda amesema serikali imegundua kupitia vyombo vya habari
mjini Nairobi kwamba Kenya imepiga marufuku uingizaji wa gesi ya kupikia kutoka nchini Tanzania kupitia mpaka wa Kenya na Tanzania.
Mkenda alisema hatua
hiyo ya Kenya ni kinyume na makubaliano ya jamii ya Afrika mashariki na
makubaliano yalioafikiwa na mataifa hayo mawili baada ya taifa hilo kuiwekea
marufuku Tanzania mnamo mwezi Mei 18, 2017.
Kulingana na Profesa Mkenda, hatua hiyo ya Kenya itaathiri
wafanyibiashara wakubwa wa kibinafsi na raia wa kawaida ambao hujipatia kipato
kupitia biashara ya kuuza gesi .
Alisema kwamba wakati wa mkutano wa Jamii ya Afrika
mashariki ambao uliwaleta pamoja mawaziri wa biashara na viwanda swala hilo
lilijitokeza.
Amesema kuwa iliamuliwa wakati wa mkutano huo ambao
ulifanyika mwezi Juni tareh2 2017 kwamba Kenya ilifaa kuondoa marufuku ili
kuafikia makubaliano hayo ya Afrika mashariki.
Wakati wa mkutano huo Kenya ilikubali kuondoa marufuku ya
ununuzi wa gesi kutoka Tanzania kupitia mpaka wa mataifa hayo mawili.
Mbali na marufuku hiyo Kenya pia imeiwekea Tanzania marufuku
ya ununuzi wa ngano swala ambalo kulingana na Mkenda ni kinyume na makubaliano
ya biashara ya Afrika Mashariki.
Hatahivyo amesema kuwa serikali itaendelea na mpango wa
kutatua tatizo hilo.
Pia katibu huyo
hakusema ni hatua gani zilizochukuliwa na serikali ya Tanzania kufikia sasa.
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, Siku ya
Jumatatu katibu maalum nchini Kenya Andrew Kamau alisema kuwa wafanyibiashara
hawataruhusiwa kununua gesi kupitia mipakani katika kipindi cha juma moja.
Hatua hiyo kulingana na Kamau ililenga kuzuia kampuni haramu
zinazouza gesi ambazo zimeathiri usalama wa taifa hilo.
Katibu huyo aliandikia barua shirika linalodhibiti kawi na
shirika la ukadiriaji ubora wa bidhaa KBS na kusema kuwa gesi yoyote ya kupikia
inayoingia nchini ni sharti ipitie Mombasa ili kubaini ni wafanyibiashara gani
ambao hawana kibali cha kuendesha biashara hiyo.


No comments: