KUKAMATWA KWA RAIS NA KATIBU WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA(TFF)
Rais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania (TFF)
Jamal Malinzi na katibu wa shirikisho hilo Celestine Mwesigwa wamekamatwa na
taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini humo.
Aidha wawili hao walipelekwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi
kisutu jijini Dar-es-salaam ambapo
walisomewa mashtaka yao kadha ikiwemo yale ya matumizi mabaya ya ofisi kwa kutumia vibaya nyaraka za shirikisho hilo
kwa kutakatisha fedha.
Pia washtakiwa hao wamepelekwa mahabusu keko kutokana na kesi hiyo kutokuwa na dhamani
kwa hiyo basi wataletwa tena mahakamani
ifikapo julai 3 mwaka huu.
Naye Msemaji wa
taasisi hiyo ya kuzuia na kupambana na rushwa Musa Misalaba amesema kuwa wawili
hao watabaki kizuiani hadi watakapo hojiwa.
Pia Misalaba amesema kuwa
idara hiyo inaendelea kuwachunguza maafisa wengine kwa madai sawa na
hayo.
No comments: