VYAMA VYA UPINZANI NCHI ZIMBABWE VYAMTAKA MUGABE KUJIUZULU
Vyama vya upinzani nchini Zimbabwe vimemtaka Rais Robert Mugabe mwenye umri wa miaka 93
kujiuzulu.
Gazeti la kibinafasi la News Zimbabwe lilimnukuu msemaji wa
chama kikuu cha upinzani cha MDC Obart Gutu akisema “Mugabe ni lazima aondoke na aiache
Zimbabwe isonga mbele chini ya uongozi mpya."
Chama cha Zanu-PF kimemteua bwana Mugabe kuwania urais mwaka
ujao licha ya kuonekana kutokuwa na afya nzuri na amekuwa madarakani tangu
mwaka 1980.

No comments: