SOMALIA IMEINGIA KWENYE HASARA BAADA YA INTANETI KUTOPATIKANA.
Waziri wa mawasiliano nchini Somalia Abdi Anshur Hassan
ametangaza kuwa tatizo la kupotea kwa intaneti kwa muda wa takribani wiki mbili sasa ni janga kubwa kwa uchumi wa
nchi hiyo.
Bwana Hassann aliiambia radio ya taifa kuwa nchi inapoteza
takriban dola milioni 10 kwa siku kutokana na kukatika kwa internet na hadi
sasa nchi imepoteza dola milioni 130.
Aidha tatizo hilo lilisababishwa na kuharibiwa kwa nyaya za
chini ya bahari zaidi ya wiki mbili zilizopita kwa mujibu wa Radio Mogadishu.
Hata hivyo Bwana Hassan amasema kuwa serikali inafanya kila
liwezekanalo ili kurejesha huduma hiyo.

No comments: