HUZUNI ULIOWAKUMBA TIMU YA NEWCASTLE UNITED.
Kiungo wa zamani
wa timu ya Newcastle United Cheick Tiote amefariki dunia akiwa na umri
wa miaka 30 baada ya kuzimia uwanjani wakati akifanya mazoezi nchini China.
Tiote alizaliwa
Ivory coast na alizanza kucheza soka la kulipwa mnamo mwaka 2005 huko nchini Ubelgiji akiwa na klabu ya Anderlecht kabla ya kuhamia Fc Twente ya Uholanzi na kucheza mechi 86 na kushinda taji la ligi ya Eredivisie msimu wa 2009 na 2010
chini ya meneja Steve Mclaren.
Mnamo mwaka 2010 Tiote ambaye ni kiungo wa kati mkabaji alihamia Newcastle United kwa malipo ya dola za Marekani milioni 3.5 na kukaa kwenye timu hiyo miaka saba na kucheza mechi 138.
Mnamo mwaka 2010 Tiote ambaye ni kiungo wa kati mkabaji alihamia Newcastle United kwa malipo ya dola za Marekani milioni 3.5 na kukaa kwenye timu hiyo miaka saba na kucheza mechi 138.
Mwaka 2011 alifunga
bao linalokumbukwa sana baada ya kusaidia timu yake Newcastle kujikwamua kutoka
4-0 chini kwenye ligi ya Premia dhidi ya
Arsenal na kutoka sare.

No comments: