WANANCHI WA UINGEREZA KUPIGA KURA LEO KWENYE UCHAGUZI MKUU.
Shughuli za
upigaji kura zitaanza majira ya saa moja asubuhi saa za Uingereza wakati huo Zaidi
ya vituo 40,000 vitafunguliwa kote nchini.
Jumla ya wabunge 650 watachaguliwa huku takribani watu
milioni 46.9 wakiwa wamejiandikisha kupiga kura
ikiwa ni ongezeko kubwa kutoka
uchaguzi wa mwaka 2015 wakati wapiga kura milioni 46.4 walikuwa
wamejiandikisha.
Kura zingine teyari zimeshapigwa kupitia njia ya posta ambayo ilichukuwa asilimia 16.4 wakati wa uchaguzi wa mwaka 2015.
Matokeo ya viti kadha
yanatarajiwa kutangazwa ifikapo usiku wa manane, huku matokeo ya mwisho
yakitarajiwa kutangazwa Ijumaa mchana.

No comments: